Ulevi watajwa kuchangia kuziba kwa mishipa ya damu

0
13

Kaimu Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma amesema mitindo ya maisha pamoja na matumizi ya vilevi, ni baadhi ya vitu vinavyochangia kuongeza hatari kwa watumiaji kukumbwa na tatizo la kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye moyo.

Dkt. Willfredius Rutahoile ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kumaliza kufanya uchunguzi na uzibuaji mishipa inayosambaza damu kwa mgonjwa wa 171 katika hospitali hiyo.

Katika hatua nyingine, Dkt Rutahoile ametoa rai kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) baada ya kubainika kuwa matibabu, uchunguzi na uzibuaji mishipa ya damu kuwa na gharama kubwa.

Send this to a friend