Ulinzi waimarishwa Arusha uzinduzi wa Royal Tour

0
43

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Justine Masejo amesema waambia hali ya ulinzi na usalama katika Jiji la Arusha ni  shwari kuelekea uzinduzi wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour

Masejo amesema kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa na hivyo kutoa fursa kwa Watanzania na dunia kufuatilia uzinduzi huo utaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Aprili 28 mwaka huu.

Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionesha dunia ukarimu huo na kuionyesha dunia kuwa Arusha ni kitovu cha utalii.

Filamu hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza Aprili 21 jijini New York, Marekani na kisha Los Angeles Aprili 23, itaoneshwa pia Zanzibar Mei 7 na Dar es Salaam Mei 8 mwaka huu.

Send this to a friend