Ulipaji kodi kwa hiari waongezeka Tanzania

0
40

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya TZS trilioni 5.151 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2021, ikiwa ni ongezeko la 17.5% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 202/21.

TRA imesema makusanyo hayo ni ufanisi wa 94.3% ambapo lengo lilikuwa ni kukusanya TZS trilioni 5.462.

Kwa mwezi Julai TRA imekusanya trilioni 1.535, Agosti trilioni 1.645 na Septemba trilioni 1.97.

Mamlaka hiyo imesema mafanikio hayo yamechangiwa na ukuaji wa ulipaji kodi kwa hiari, kasi ya ulipaji malimbikizo, kuimarika kwa uhusiano baina ya wananchi na TRA kufuatia utatuzi wa migogoro nje ya mahakama.

Sababu nyingine ni kuimarika kwa biashara za kimataifa kutokana na kutolewa kwa chanjo ya UVIKO19 na imani kwa wafanyabiashara kufuatia serikali kuendelea kutimiza miradi mikubwa kama SGR na bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

Send this to a friend