Ummy: Wanaorudia vipimo wanaidhoofisha NHIF

0
43

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? Ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.

Send this to a friend