Unahisi makampuni mengine ya simu yataweza kuipiku INFINIX NOTE 12 VIP?

0
49

Leo tuangazie simu mpya na bora ya Infinix NOTE 12 VIP, na mwishowe tutajua ni kwanini ununue Infinix NOTE 12 VIP badala ya simu za makampuni mengine kama Samsung A53 au Oppo Reno 7 kwa kuangalia sifa za ndani na njee pamoja na bei za simu hizi.

CAMERA

Tukianza na camera simu ya Infinix NOTE 12 VIP ina camera yenye MP 108 huku ikiwa na teknolojia za kisasa zaidi kufanya kukupa picha nzuri zaidi na angavu na Reno 7 pamoja na Samsung A53 zikiwa na MP 64MP na hii kuifanya Infinix NOTE 12 VIP kuwa na picha zenye quality bora zaidi kulinganisha na Samsung na Reno 7.

BETRI

Kwa upande wa betri simu ya Infinix NOTE 12 VIP ina 4500mAh na teknolojia ya 120W Fast Charging, teknolojia inayoifanya simu hii kuwa simu ya kwanza kuwa na uwezo wa kujaza 100% simu ndani ya dakika kumi na saba (17 Minutes) huku Samsung A53 ikiwa na battery la ujazo mkubwa zaidi la mAh 5000 lakini teknolojia ya kujaza chaji ni ndogo ikiwa ni 25watt ambapo mtumiaji atahitaji kuanzia lisaa limoja ili kufikia asilimia 100.

Teknolojia ya kujaza chaji kwa haraka ni teknolojia ya kisasa na kwa kuzingatia viwango vya dunia vya simu kujaa chaji, Hapa Infinix NOTE 12 VIP imeongoza kwa kuwa simu ambayo inaweza kujaa chaji kwa haraka zaidi ya simu zote unazozijua dunia na si kwa Samsung A53 au Oppo Reno 7.

Maboresho haya pia yanaenda sambamba na kuifanya betri ya Infinix NOTE 12 VIP kutokuwa na ugonjwa wa kuvimba au kuwaka sana moto pindi unapoitumia kwa muda mrefu kama baadhi ya simu zingine duniani ambapo betri yake inawaka moto kadri unazidia kuitumia simu yako muda mrefu.

Lakini kubwa kuliko ni kuwa teknolojia hii haina madhara ya kiafya kwa mtumiaji hivyo kumuepusha mtumiaji na madhara yanayosababishwa na miale ya mionzi ya betri la simu.

STORAGE

Simu hizi zote zinastorage ya kutosha zote zikiwa na Rom ya GB256 kwajili ya kuhifadhi picha na matukio mengine mbalimbali isipokuwa katika kipengele cha kuwasilisha mawasiliano ili processor iweze kufanya kazi kwa haraka kitaalamu Ram Infinix imekuja na 13GB (8GB+5GB RAM Fusion) na Samsung ikiwa na Ram ya GB 8 ivyo Infinix NOTE 12 VIP inafanya mawasiliano kwa haraka zaidi na kufanya uchakataji wa kazi uwe wa haraka na si wenye kuhitaji chaji nyingi.

KIOO

Infinix NOTE 12 VIP, Reno na Samsung A53 wigo wake a mbele ni kioo aina ya AMOLED ambacho ni kioo super ukilinganisha na kioo kama IPS lakini tofauti haiwezi kosekana Infinix NOTE VIP pamoja ya kuwa kioo chake ni AMOLED lakini pia kina uwezo wa kuonyesha aina Bilioni 1 za Rangi na kufanya picha zinazochukulia na simu ya Infinix NOTE 12 kuwa na uhalisia mkubwa.

BEI

Kulingana na uchambuzi huo hapo juu, moja kwa moja unaweza kusema hapo simu ghari zaidi ni Infinix NOTE 12 VIP ila ukweli ni kuwa ni tofauti, Infinix NOTE 12 VIP inapatikana kwa Tsh. 820,000/=, Samsung 875,000/= na Reno 7 890,000/=. Je Samsung na Oppo wataweza kujibu haya mashambulizi kutoka Infinix? Weka comment yako.

 

 

Send this to a friend