UNAIDS yatabiri ongezeko la maambukizi ya Ukimwi Marekani ikiendelea na usitishwaji wa misaada

0
2

 Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi (UNAIDS) limesema kesi mpya za maambukizi ya HIV na Ukimwi huenda zikaongezeka kwa zaidi ya mara 6 kufikia 2029 ikiwa Marekani itaendelea kusitisha ufadhili wa misaada .

 UNAIDS imesema maambukizi ya HIV yamekua yakishuka miaka ya hivi karibuni, huku maambukizi mapya yakiwa milioni 1.3 pekee 2023, ikiashiria kushuka kwa asilimia 60 tangu rekodi kubwa ya maambukizi ya 1995.

 Kiongozi wa UNAIDS, Winnie Byanyima amesema kufikia mwaka 2029, huenda kukawa na maambukizi mapya milioni 8.7, ongezeko la vifo mara 10 hadi watu milioni 6.3, ikiwa na maana ya ongezeko la yatima milioni 3.4.

Byanyima ameiomba serikali ya Marekani kutositisha msaada wake ghafla kwa kuwa hatua hiyo imezua hofu na wasiwasi miongoni mwa mataifa mengi ya kiafrika, yaliyoathiriwa zaidi na Ukimwi.

Rais Donald Trump ametangaza kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Hatua hiyo ilitajwa kuwa ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo.

Send this to a friend