Unawezaje kupata fedha zilizoachwa na marehemu kwenye simu yake?

0
54

Inawezekana umempoteza ndugu yako na unahitaji kutoa akiba ya fedha iliyoko kwenye simu ya marehemu, lakini haufahamu nywila zake ili uweze kufanya muamala.

Hizi ni nyaraka muhimu unazotakiwa kuwa nazo ili kufanya muamala katika simu ya ndugu yako aliyefariki.

1. Hati ya usimamizi wa mirathi
Kwa Wakristo ni fomu namba 68, na kwa Waislamu ni fomu namba 4, nyaraka hizi hupatikana mahakamani baada ya kukamilisha utaratibu wa miradhi.

2. Cheti cha kifo cha ndugu yako (Death Certificate) kinachopatikana katika ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)

3. Kiapo cha msimamizi wa mirathi. Hiki hupatikana katika ofisi ya wakili yeyote.

4. Wosia kama upo ila kama haupo sio lazima.

5. Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya mtaa.

6. Kitambulisho cha msimamizi wa mirathi. Kinaweza kuwa cha Taifa (NIDA) au kitambulisho cha mpiga kura, leseni ya udereva, hati ya kusafiria (passport).

7. Muhtasari wa kikao cha familia ambao hupatikana baada ya familia kukaa, kuunda na kufikia makubalilano.

8. Kitambulisho cha mtu aliyefariki dunia, kinaweza kuwa cha NIDA, cha mpiga kura au leseni.

Kimsingi, kitu kikubwa zaidi kinachohitajika katika kufuatilia mirathi iliyoko kwenye akaunti ya simu ya ndugu aliyefariki ni hati ya usimamizi wa mirathi.

Hivyo, baada ya kupeleka nyaraka hizo kwenye ofisi za mtandao husika, utapewa namba ya siri ya akaunti ya simu ya ndugu yako aliyefariki dunia kisha kufanya miamala au kuangalia kama kuna akiba yoyote.

Send this to a friend