Upelelezi wa kesi ya aliyekuwa kocha wa makipa Simba na wenzake umekamilika

0
52

Upelelezi wa kesi ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Heroine kilogramu 34.89 inayomkabili aliyekuwa kocha wa makipa wa klabu ya Simba, Muharami Sultan (40) na wenzake watano umekamilika.

Wakili wa Serikali, Carolina Matemu ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi mbele ya hakimu mkuu, Mary Mario kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika, na tayari wamepeleka taarifa mahakama kuu ili waweze kuwasomea maelezo ya mashahidi.

Aidha, Wakili Matemu ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo, hata hivyo ombi hilo limekubaliwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 16 mwaka huu.

Muharami na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Novemba 21, 2022 wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha heroine yenye uzito wa kilo 34.89 jijini Dar es Salaam.

Send this to a friend