Upigaji kura Zanzibar kufanyika siku mbili

0
65

Wananchi visiwani Zanzibar wanatarajia kupiga kura kwa siku mbili katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wananchi wote watapiga kura ya Oktoba 28, lakini siku moja kabla, Oktoba 27 kutakuwa na zoezi la kupiga kura ya mapema ambayo itahusisha makundi yote yatakayohusika kusimamia uchaguzi Oktoba 28.

Kwa mujibu wa kifungu cha 82 cha Sheria ya Uchaguzi namba yam waka 2018 upigaji kura ya mapema utawahusisha watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi siku ya uchaguzi.

ZEC imesema uchukuaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa ngazi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani utakuwa kati ya Agosti 26 hadi Septemba 9, na uteuzi utakuwa Septemba 10 mwaka huu.

Vyama vya siasa visiwani humo vimesema vipo tayari kwa uchaguzi mkuu, kwani vimekamilisha maandalizi yanayohitajika.

Send this to a friend