Upinzani Afrika Kusini kuishitaki Serikali kutokana na kukatika umeme

0
35

Vitisho vya kuishtaki serikali kutokana na kukatika kwa umeme nchini Afrika Kusini vimetolewa na makundi ya upinzani, chama cha wafanyakazi na wamiliki wa makampuni.

Serikali ya Afrika Kusini imepewa muda hadi kufikia Ijumaa watatue tatizo hilo la kukatika kwa umeme la sivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa kukiuka wajibu wake wa kutoa huduma hiyo.

Aidha, wameandika barua ya madai kwa Waziri wa Mashirika ya Umma, Pravin Gordhan na mtendaji mkuu wa kampuni ya shirika la serikali ya Eskom, Andre de Ruyter, wakisema kuwa serikali inakiuka wajibu wake wa kutoa umeme.

Ramaphosa asitisha safari ya Uswisi kutokana na mgao wa umeme

Siku ya Jumatatu Januari 16, 2023 wakaazi wa Boksburg waliingia mitaani kuandamana kupinga kukatika kwa umeme kwa saa nyingi ambapo inadaiwa hivi majuzi umeme ulikatwa karibia hadi saa 10 kila siku.

Send this to a friend