Upinzani Ghana kuipinga tozo ya miamala mahakamani

0
35

Upinzani nchini Ghana umesema kwamba utakwenda Mahakama ya Juu kupinga kodi mpya iliyoanzishwa kwenye miamala ya simu.

Kodi hiyo mpya ya miamala ya kieleketroniki (E-Levy) ilipitishwa na bunge la nchi hiyo jana chini ya hati ya dharura.

Tozo hiyo inaelekeza kukatwa asilimia 1.5 ya muamala utakaofanyiwa, ikiwa ni punguzo la asilimia 0.25 kutoka kiwango cha asilimia 1.75 kilichokuwa kinapendekezwa.

Wabunge wa upinzani waligoma kushiriki kwenye mchakato wa kura na kutoka nje ya bunge wakidai kuwa kodi hiyo haikuwa halali.

Waziri wa Fedha nchini humo, Ken Ofori-Atta alitetea muswada huo akisema kwamba wanatarajia kukukusanya mapato TZS trilioni 2.1.

Mbali na hatua hiyo katika kukabiliana na mdoororo wa uchumi unaosababishwa na UVIKO19 na vita vya Urusi na Ukraine, serikali ya nchi hiyo pia imepunguza mishahara ya baadhi ya watumishi.

Send this to a friend