Usafiri wakwamisha Mbowe kufikishwa mahakamani

0
52

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi wameshindwa kufikishwa mahakamani leo kutokana na tatizo la usafiri gerezani.

Hayo yameeleezwa na Wakili wa Jamhuri, Pius Hila wakati kesi hiyo iliyofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa ajili ya kutajwa ikiendelea.

Kutokana na watuhumiwa hao kutokuwepo mahakamani kesi hiyo imendeshwa kwa njia ya video conference.

Hata hivyo wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala ameiomba mahakama kuhakilisha kuwa watuhumiwa hao wanafikishwa mahakamani badala ya kesi kufanyika kwa njia ya mtandao.

Katika kesi ya msingi Mbowe na anatuhumiwa kufadhili vitendo vya kihalifu na kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi vinavyohatarisha usalama wa nchi na kutia hofu wananchi. Anatuhumiwa kutenda makosa hayo kati ya Mei na Agosti 2020 katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Dar es Salalaam na Morogoro.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 27 mwaka huu itakapofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.

Wakati huo huo, Kibatala amewasilisha taarifa ya kusudio la kuomba mahakama kupeleka Mahakama Kuu suala la kikatiba linalohusu taasisi moja hapa nchini kutokana na matamshi yake yaliyowafanya wateja wake kujiona kwa wamekutwa na hatia.

Send this to a friend