Ushuru mpya wa Trump watikisa masoko ulimwenguni

0
3

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ushuru mpya kwa bidhaa zote zinazoingia nchini humo, kiwango cha chini kikiwa asilimia 10, huku baadhi ya nchi zikikabiliwa na ushuru wa hadi asilimia 50.

Umoja wa Ulaya utatozwa asilimia 20, Japan asilimia 24, Mexico na Canada asilimia 25 iliyowekwa awali, India asilimia 26, China asilimia 34, huku nchi maskini kama Vietnam na Mynmar zitatozwa hadi ushuru wa asilimia 50.

Trump amesema ushuru huo unalenga kushughulikia miaka mingi ya biashara isiyo ya haki ambayo imeathiri Marekani. Ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa zote utaanza kutumika tarehe 5 Aprili, mwaka huu.

“Tutaifanya Marekani kuwa kubwa na tajiri tena. Nchi yetu imenyang’anywa kwa zaidi ya miaka 50. Hilo halitafanyika tena,” amesema.

Hatua hiyo imeleta mtikisiko katika masoko ya dunia, huku masoko ya Asia yakishuka kwa kasi.

Send this to a friend