Utafiti: Asilimia 21 ya wanawake Tanzania wamechepuka

0
15

Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022, asilimia 21 ya wanawake wameshiriki ngono na wanaume ambao sio wenza wao na wala hawaishi nao. Kati ya hao, asilimia 22 walitumia kinga mara ya mwisho waliposhiriki ngono na watu hao.

Kwa upande wa wanaume, ripoti imebainisha kuwa asilimia 38 ya wanaume wameshiriki ngono na wanawake ambao sio wenza wao na wala hawaishi nao, na kati ya hao, asilimia 43 walitumia kinga mara ya mwisho waliposhiriki ngono na wapenzi hao.

Aidha, ripoti imetaja asilimia 4 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wameshiriki ngono na mpenzi zaidi ya mmoja katika kipindi cha miezi 12 kabla ya utafiti huku takribani robo ya wanaume (asilimia 23) wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wameshiriki ngono na mpenzi zaidi ya mmoja katika kipindi hicho.

Nchi za Kiafrika zenye kiwango cha juu zaidi cha talaka

Kwa upande wa upimaji wa Virusi vya UKIMWI, wanawake 8 kati ya 10 wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamewahi kupima VVU na kupata majibu yao ikilinganishwa na asilimia 64 kwa wanaume.

Send this to a friend