Utafiti: Asilimia 30 ya watu nchini wana tatizo la ugumba

0
39

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema imejipanga kupitia upya gharama za upandikizaji wa mimba kwa wananchi wenye matatizo ya kutopata watoto ili kuwapunguzia gharama hizo.

Ameyasema hayo Waziri Ummy Mwalimu wakati akitembelea Taasisi ya Kairuki mkoani Dar es Salaam ambayo inatoa huduma ya upandikizaji mimba ambapo ameeleza kuwa tatizo la ugumba ni kubwa nchini lakini mpaka sasa hakuna takwimu rasmi za kitaifa.

Ameongeza kuwa katika utafiti mdogo uliofanyika umeonesha asilimia 30 ya watu nchini wana tatizo la ugumba, huku duniani inakadiriwa kuwa katika kila mahusiano ya wenza wanne, mmoja kati yao anakumbwa na tatizo la hili.

Isome hapa ripoti ya Wizara ya Afya kuhusu watumishi walioonekana kwenye video wakizozana

Aidha, Waziri Ummy amesema Serikali itaangalia uwezekano wa kuweka nusu ya gharama hizo katika vifurushi vya bima ya afya kwa wote ili kuwapunguzia wananchi gharama za kupata huduma hiyo.

Kituo cha upandikizaji mimba cha Kairuki kinatoa huduma hiyo kwa gharama ya kuanzia shilingi milioni 13 hadi milioni 17 kutegemea na aina ya huduma inayohitajika.

Send this to a friend