Utafiti: Dar yaongoza kwa wanawake kuharibikiwa mimba

0
90

Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2022 yanaonesha kuwa asilimia 23 ya mimba katika mkoa wa Dar es Salaam ziliharibika na kufanya mkoa huo kuwa na kiwango cha juu zaidi cha kuharibika kwa mimba kuliko mikoa yote nchini.

Ripoti hiyo ya utafiti iliyozinduliwa Oktoba 28 mwaka huu na Rais Samia Suluhu Hassan imehusisha wanawake 15,254 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 kutoka kwenye kaya 15,705 waliofanyiwa mahojiano na kutolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

Matokeo hayo yameonesha kuwa taarifa za ujauzito kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 15 ha 49 kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya utafiti huo, asilimia 90 walijifungua watoto hai na asilimia 10 walipoteza ujauzito.

Aidha, kati ya waliopoteza ujauzito, asilimia nane mimba zao ziliharibika, asilimia mbili walijifungua watoto wafu na asilimia chini ya moja walitoa mimba huku mkoa wa Rukwa ukiongoza kwa kiwango cha chini zaidi cha mimba kuharibika.

Send this to a friend