Utafiti: 'Diet soda' zinavyosababisha magonjwa ya moyo, kisukari na kiharusi

0
37

Utamu wa bandia (artificial sweeteners) ni moj ya vioungo muhimu san katika uandaaji wa soda za lishe (diet soda). Lakini tafiti zimeonesha kuwa utamu bandia ndani ya soda hizo unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Mwanzoni mwa miaka ya 1960 kinywaji hicho kiliingia sokoni kwa lengo la kuwasaidia wale wote waliotaka kupunguza matumizi ya sukari ili kuweza kupunguza uzito kutokana n kuwa na kiwango kidogo sana cha sukari na kalori.

Lakini kuihalisia, mwili huwa na wakati mgumu sana katika kutambua kama soda moja ni ya lishe na nyingine ni ya kawaida, kama ambavyo baadhi ya watu pia hushindwa kufanya hivyo.

Mtu anapokula au kunywa kitu chochote chenye utamu, ubongo wake hutuma taarifa kwenda kwenye kongosho ambalo huzalisha insulini inayotumika kuhifadhi sukari katika seli zetu kwa ajili ya kuupa mwili nguvu.

Hivyo mtu anapokunywa soda ya lishe, utamu wake hudanganya miili yetu kudhani kuwa ni sukari ya kawaida, lakini sukari hiyo isipofika kama ambavyo mwili umejiandaa kuipokea, insulini inakuwa haina cha kuhifadhi.

Wanasayansi wanaamini kuwa kuudanganya mwili wako kwa njia hii kila mara unywapo soda hiyo, ndiko kunapopelekea soda hizo kuhusishwa na shinikizo la juu la damu, kupanda kwa sukari, na kuongezeka uzito, mambo ambayo yanaongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, kisukari na kiharusi.

Utafiti mmoja umebaini kuwa wanyaji wa soda za lishe wako hatarini zaidi kupata matatizo ya moyo kuliko wanywaji wa soda za kawaida.

Pia imeelezwa kuwa unywaji wa soda za lishe wakati wa chakula ndio mbaya zaidi kwa sababu kalori feki katika soda zinaweza kuudanganya mwili kuhusu kiwango halisi cha kalori ambacho mtu amekula, na hivyo kuathiri kiwango cha kalori ambacho kitameng’enywa, na hivyo huweza kuacha baadhi ya kalori nje ambazo huhifadhiwa kama mafuta.

Jambo lingine ni kuwa utamu bandia katika soda hizo unaweza kuwa kuzidi kwa kiwango kikubwa utamu wa soda za kawaida, hivyo unapokunywa ubongo unatambua kuwa kuna kalori nyingi sana, jambo ambalo si kweli. Kutokana na mwili kujiandaa kwa kiwango kikubwa, lakini haupati kile ulichotarajia, ndipo mtu hujikuta akitamani kunywa soda nyingine, na nyingine, jambo ambalo ni hatari zaidi.

Inashauriwa kujikita zaidi kunywa maji kama sababu inayokufanya unywe soda za lishe ni kupunguza uzito.

Send this to a friend