Utafiti: Hali ya umasikini Tanzania imepungua

0
16

Tanzania imetajwa kuwa kwenye kiwango kizuri cha upatikanaji wa chakula kutokana na kuwepo kwa takwimu sahihi za hali ya maisha katika kaya, hali iliyopelekea kiwango cha umasikini wa chakula kushuka nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (LSMS-ISA), uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema Programu hiyo ya utafiti iliyoanza 2008 ambayo ilifadhiliwa na Benki ya Dunia, imeweka alama sio tu katika uzalishaji wa takwimu muhimu za hali ya maisha katika kaya bali pia takwimu zilizozalishwa zimekuwa nyenzo muhimu za kutathmini sera na programu zinazotekelezwa na Serikali, taasisi binafsi na wadau wa maendeleo.

“Kiwango cha umasikini kwa sasa kimepungua hasa umasikini wa upatikanaji wa chakula, chakula kipo kwa wingi cha kutosha ambapo sisi watanzania leo tunalisha mpaka nchi jirani” amesema Chande.

Naye, Kamishna wa Sensa, Anna Makinda, amewataka watafiti kurudisha tafiti hizo kwa wananchi kwa maana wao ndio wahusika wakuu na kueleza kuwa utafiti huo umefanikiwa kwa sababu umeweza kumfikia mtu mmoja mmoja na kuelezea ukweli kuhusu maisha yake.

Send this to a friend