Utafiti: Jeshi la Polisi lashika namba 1 kwa rushwa nchini

0
60

Takwimu iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imeitaja Jeshi la Polisi kama Sekta inayoongoza kwa vitendo vya rushwa zaidi nchini ikiongoza kwa asilimia 45.6 na kufuatiwa na Sekta ya Afya kwa asilimia 17.9.

Takwimu hiyo ya Septemba, 2020 inaitaja pia Mahakama ya Sheria kushika nafasi ya tatu kwa asilimia 11.9 huku Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikishika nafasi ya nne kwa asilimia 6.1.

Kamati yaundwa kuchunguza matokeo ya Shule Kuu ya Sheria

Aidha, taarifa ya TAKUKURU imesema kiwango cha rushwa kimeonekana kuwa cha chini, ambapo asilimia 87.7 ya waliohojiwa waligundua kuwa viwango vya rushwa vimepungua kati ya mwaka wa fedha 2014/2015 na 2019/2020.

Taarifa ya utafiti inaonesha wanaume wako kwenye nafasi kubwa ya kuombwa kutoa hongo isipokuwa katika huduma za afya ambapo wanawake wana uwezekano mkubwa wa kutoa rushwa kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na asilimia 3.1 kwa wanaume.