Utafiti: Kuongeza chumvi mezani kunapunguza umri wa kuishi

0
43

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tulane huko New Orleans umebaini kuwa, kuongeza chumvi kwenye chakula mezani kunaweza kupunguza umri wa kuishi.

Katika utafiti uliohusisha zaidi ya washiriki 500,000 nchini Uingereza, watafiti waligundua kuwa, kuongeza chumvi mezani kunapunguza umri wa kuishi wa mwanaume kwa miaka miwili na mwanamke hupungua mwaka mmoja na nusu.

Utafiti umeonesha kuwa wale ambao kila mara waliongeza chumvi kwenye chakula chao, walikuwa na hatari ya asilimia 28 ya kufariki mapema ikilinganishwa na wale ambao hawakuongeza chumvi au walifanya hivyo mara chache sana.

“Kwa ufahamu wangu, utafiti wetu ndio wa kwanza kutathmini uhusiano kati ya kuongeza chumvi kwenye vyakula na kupungua kwa umri wa kuishi,” amesema Profesa wa Chuo Kikuu Tulan Lu Qi.

Profesa ameeleza kwamba, kuongeza chumvi mezani ni tabia ya kawaida ya ulaji ambayo inahusiana moja kwa moja na mazoea ya mtu ya muda mrefu.

Hata hivyo, watafiti waligundua kuwa watu ambao walikuwa na mazoea ya kuongeza chumvi mezani walipunguza mazoea hayo kwa sababu ya kutumia kiasi kikubwa cha matunda na mbogamboga.

Send this to a friend