Utafiti Mpya: Unywaji pombe wa wastani hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo

0
46

Uafiti umeonesha kuwa watu wanaotumia kiwango cha wastani cha pombe chini ya chupa moja  kwa siku kwa wanawake, na chupa moja hadi mbili kwa siku kwa wanaume wana hatari ndogo ya magonjwa makubwa ya moyo na mishipa.

Magonjwa hayo yaliyobainishwa ni kama vile mshtuko wa moyo na kiharusi ambayo yana asilimia chache ya kuwapata watumiaji wa wastani ikilinganishwa na watu wanaojiepusha na unywaji wa pombe kabisa pamoja na wale wanaokunywa pombe kupitiliza.

Hata hivyo, tafiti imeeleza kuwa pombe huongeza viwango vya HDL, cholesterol nzuri, na wanywaji wana viwango vya chini vya protini yenye kunata iitwayo ‘fibrinogen’ katika damu, ambayo inaweza kupunguza hatari ya kuganda kwa damu.

Mtafiti, na mkurugenzi-mwenza wa Kituo cha Utafiti wa Picha za Moyo na Mishipa katika Hospitali Kuu ya Massachusetts, Dk. Ahmed Tawakol amebainisha kuwa baada ya kunywa pombe kidogo, mtumiaji anaweza kuhisi utulivu.

Pia uchunguzi huo uliohusisha uchanganuzi wa ubongo wa mamia ya watu umegundua kwamba wale ambao walikuwa wanywaji pombe wa wastani walikuwa wamepunguza mkazo (stress) katika ‘amygdala’, sehemu ya ubongo ambayo hushughulikia hofu na vitisho pamoja na mashambulizi machache ya moyo na viharusi.