UTAFITI: Sababu kuu 5 zinachopelekea rushwa ya ngono vyuoni

0
106

Mjadala kuhusu rushwa ya ngono umeshika kasi hasa kwenye mtandao wa Twitter kwa siku mbili sasa. Mvutano mkubwa ukiwa katika kubainisha chanzo hasa cha tatizo hilo ambalo mbali na kuwa na athari za kiafya, linapelekea kuwa na wahitimu wasio na sifa.

Mwaka 2020 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya utafiti katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma kuhusu tatizo hilo ambalo pamoja na  mambo mengi, ulitaka kubainisha chanzo cha tatizo.

Watu mbalimbali waliohojiwa na kwa ujumla sababu tano zilibainika kuchochea tatizo hilo, ambazo ni;

1. Ukosefu wa maadili

2. Ushawishi wa mtu mwenye mamlaka

3. Mfumo wa utoaji taarifa kutokuwa rafiki

4. Mifumo dhaifu kushughulikia rushwa ya ngono

5. Mamlaka ya kutoa alama za mitihani kuachwa chini ya walimu pekee.

Hapa chini ni utafiti huo, unaweza kusoma kufahamu mengi zaidi kuhusu hali ya rushwa ya ngono vyuoni.

[pdf-embedder url=”https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2021/10/RUSHWA-YA-NGONO-FINAL-JULAI-2020.-3.pdf” title=”RUSHWA YA NGONO FINAL -JULAI-2020.-3″]