Utafiti: Utazamaji wa video za ngono mitandaoni unavyosababisha uchafuzi wa mazingira
Utazamaji wa video za ngono mitandaoni huzalisha carbondioxide tani milioni 81 kwa mwaka, sawa na inayozalishwa na gesi hiyo nchi 72 zenye uchafuzi mdogo, na hivyo kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya uchafuzi wa mazingira.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Shift Project la nchini Ufaransa umebainisha kuwa gesi hiyo hutokana nguvu kubwa ya umeme inayohitajika kusukuma mitambo ili video hizo ziweze kuonekana kwa watazamaji.
Shirika hilo limesema video hizo hutazamwa ama kwenye simu au kompyuta, hivyo nguvu kubwa sana huhitaji kuhakikisha maudhui hayo yanafika kwenye vifaa hivyo.
Mwaka 2016 PornHub ilitumia nguvu ya umeme zaidi kilowati milioni 6 kuendesha mitambo yake ya video hiyo, na kiwango hicho huongezeka kila mwaka.
Shirika hilo linashinikiza kupunguzwa kwa ukubwa wa video zinazowekwa mtandaoni, ili kupunguza nguvu itakayotumika kuzifikisha kwa walaji wa mwisho, pamoja na matumizi ya video hizo.
Shift Project imesema kuwa haishabikii au kupinga video hizo, lakini kikubwa na kuangalia athari zinazotokea katika mazingira.
Tovuti zinazoonesha picha za ngono hutembelewa na watu wengi zaidi kuliko wanaotembelea Netflix, Twitter na Amazon kwa pamoja.
Mwaka 2018, watizamaji wa video hizo walitumia saa 5,517,000,000 kutizama video hizo katika tovuti ya PornHub.