Utafiti: Vijana wanaokunywa pombe peke yao hatarini kuto acha wakiwa watu wazima

0
51

Utafiti mpya umebaini kuwa kunywa pombe ukiwa peke yako wakati wa ujana kunaweza kuongeza hatari ya matumizi mabaya ya pombe pindi unapokuwa mtu mzima, hasa kwa wanawake.

Mwandishi mkuu wa utafiti, Kasey Creswell, Profesa Msaidizi wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon huko Pittsburgh, Pennsylvania amesema wanawake wengi husumbuliwa na mahusiano yanayosababisha upweke na kuwapelekea kunywa pombe wakiwa wamejifungia ndani.

Mwanafunzi ajiteka mwenyewe ili kupata fedha kwa wazazi

“Sababu kuu ya vijana kunywa peke yao ni kukabiliana na hisia hasi, na kutafuta unafuu wa kukabiliana na hali wanazozipitia, hivyo husababisha matumizi mabaya ya pombe hapo baadaye na hata husababisha shida zaidi zinazohusiana na pombe,”amesema.

Aidha, utafiti umeonesha unywaji pombe wa peke yako unaongeza hatari ya ugonjwa wa matumizi ya pombe kwa asilimia 35% na kukufanya usiache hata inaposababisha madhara ya kimwili au kihisia kwa mnywaji au wengine.

Tafiti zinaeleza kuwa mtu anayekunywa pombe peke yake ana asilimia kubwa ya kutoacha pindi atakapokuwa mtu mzima ikilinganishwa na yule anayekunywa pombe na watu wengine.

Uchunguzi pia umeandika ongezeko hilo linasababishwa na mfadhaiko, hisia mbaya na matatizo ya afya ya akili kwa vijana wengi.

Send this to a friend