Utafiti: Wagonjwa wa moyo ambao hawajaoa wako hatarini zaidi kufariki

0
42

Watafiti wamegundua kwamba wagonjwa ambao hawajaoa na wenye matatizo ya moyo wako kwenye hatari zaidi wakilinganishwa na wagonjwa walio katika ndoa.

Watafiti katika Jumuiya ya Ulaya ya Magonjwa ya Moyo wanaeleza kwamba tofauti hizi zinaweza kuchangia kupunguza viwango vya maisha  kwa wagonjwa ambao hawako kwenye ndoa.

Kulingana na Dkt. Fabian Kerwagen wa Kituo Kikuu cha Kushindwa kwa Moyo katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Wurzburg nchini Ujerumani wanandoa wanaweza kusaidiana kuondokana na msongo wa mawazo, kupeana faraja ikilinganishwa na wagonjwa ambao hawako kwenye ndoa.

“Tuligundua kwamba wagonjwa ambao hawako kwenye ndoa walionesha mwingiliano mdogo wa kijamii kuliko wagonjwa walioko kwenye ndoa na hawakuwa na ujasiri wa kudhibiti hali ya kushindwa kwao kwa moyo,” amesema Dkt. Fabian.

Ametoa ushauri kwa madaktari kuwauliza wagonjwa wenye matatizo hayo ikiwa wako kwenye ndoa au la, ili kutoa ushauri utakaowasaidia kuziba mapengo hayo.

Send this to a friend