Utafiti: Waliougua UVIKO19 hatarini kupata upungufu wa nguvu za kiume

0
38

Wizara ya Afya imesema utafiti umebaini kuwa wanaume waliougua ugonjwa wa UVIKO-19 wako katika hatari ya kupata upungufu wa nguvu za kiume.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dk Baraka Nzobo kutoka Wizara ya Afya wakati wa kampeni ya kuhamasisha jamii kuchanja, amewashauri wanaume kuchukua hatua za haraka ili kupata chanjo kuepuka tatizo hilo.

Aidha, Dkt. Nzobo amesema Serikali imetoa chanjo na wataalam wapo, hivyo wananchi wajitokeze kuchanja kwani itakuwa ni jambo jema kwa kuwa magonjwa mengi yameweza kudhibitiwa kupitia chanzo.

“Tujitokeze na tuachane na imani potofu ambazo hazina ukweli katika jamii zetu, pia wale wanaosita jitokezeni kuchanja chanjo hii,” amesema Nzobo.

Send this to a friend