UTAFITI: Wanaokula udongo wanaugua ugonjwa wa akili

0
22

Mwanasaikolojia Charles Kalungu kutoka shirika la Psychezone International amesema watu wanaopendelea kula vitu visivyo chakula na visivyo na manufaa yoyote ya kilishe wanasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia ambalo kitaalamu linaitwa Pica.

Amesema tatizo hilo mara nyingi huwakumbua watoto, vijana na wajawazito. Ameongeza kuwa wakati mwingine mtu anayesumbuliwa na tatizo la kuchanganyikiwa huweza kula vitu hivyo kama njia ya kutuliza hasira au maumivu aliyonayo.

Vitu hivyo ni pamoja na mchele, udongo, mkaa, na wengine huenda mbali hadi kula kinyesi kutokana na upungufu wa virutubisho.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kinamama na uzazi, Cyril Masawe amesema sio wanawake wajawazito wote wanaokula udongo na vitu vinginevyo na kwamba inapotokea, inachangiwa na mabadiliko ya homoni, hivyo anatakiwa kufanyiwa vipimo kwa sababu hicho ni kiashiria cha upungufu wa madini mwilini.

Amesisitiza kuwa hali hiyo siyo salama kwa wajawazito kwa sababu anaweza akasababisha kuwa na minyoo, na hivyo kumletea mtoto madhara. Pia udongo unaweza kuwa na madini kama vile risasi, arsenic, aluminiamu na kuhatarisha afya ya mama na mtoto.

Wataalamu wamesema kuwa wenye tatizo hilo wanatakiwa kufika hospitalini haraka kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini chanzo ni nini.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend