Utafiti: Wanawake huathirika zaidi na uchafuzi wa hewa kuliko wanaume

0
12

Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Manitoba, Winnipeg, Kanada umebaini kuwa athari za uchafuzi wa hali ya hewa huenda zikawa kali zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.

Watafiti walitafuta mabadiliko katika damu ya watu yanayosababishwa na moshi wa dizeli. Katika wanawake na wanaume, walipata mabadiliko katika vipengele vya damu vinavyohusiana na kuvimba, maambukizi na ugonjwa wa moyo na mishipa, lakini mabadiliko hayo yalipatikana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.

“Tayari tunajua kwamba kuna tofauti za kijinsia katika magonjwa ya mapafu kama vile pumu na maambukizo ya kupumua. Utafiti wetu uliopita ulionyesha kuwa moshi wa dizeli husababisha uvimbe kwenye mapafu na huathiri jinsi mwili unavyoshughulika na magonjwa ya kupumua. Katika hili tulitaka kuangalia athari zozote kwenye damu na jinsi zinavyotofautiana kwa wanawake na wanaume.” amesema mtafiti Dkt. Hemshekhar Mahadevappa.

Mtaalamu amesema utafiti huo ulihusisha watu kumi wa kujitolea, watano wa kike na watano wa kiume ambao wote walikuwa na afya njema na wasiovuta sigara. Kila mtu alitumia saa nne kupumua hewa iliyochujwa na saa nne kupumua hewa iliyo na moshi wa dizeli, lakini utafiti ulibaini, wanawake walionekana kuathirika zaidi kuliko wanaume.

Send this to a friend