Utafiti: Wanawake wanaoweka nywele dawa hatarini kupata saratani ya mfuko wa uzazi

0
71

Utafiti mpya kutoka Chuo Kikuu cha Boston unaonyesha kwamba wanawake wanaoweka dawa kwenye nywele (hair relaxers) zaida ya mara mbili kwa mwaka au kwa zaidi ya miaka mitano wanaweza kuwa na ongezeko la asilimia 50 ya hatari ya saratani ya mfuko wa uzazi.

“Hizi dawa za kunyosha nywele tayari zimehusishwa na saratani ya matiti, saratani ya ovari na sasa saratani ya mfuko wa uzazi,” anasema Dkt. Onyinye D. Balogun, daktari wa mionzi oncologist katika Hospitali ya NewYork-Presbyterian Brooklyn Methodist ambaye ameongeza kuwa “ingawa ushahidi zaidi unahitajika, tunahitaji kusimama na kutilia maanani kwa karibu.”

Kwa mujibu wa Dkt. Balogun anasema bidhaa hizi zimejaa kemikali, na baadhi zinaweza kuunganishwa na formaldehyde ambayo imekuwa ikichukuliwa kama kemikali ya kansa na ni kemikali ileile anayotumika kuhifadhi maiti.

P2 inavyosababisha madhara kwenye hedhi na mifupa

“Tunadhani wakati zinapotumiwa kwenye nywele, zinaweza kufyonzwa moja kwa moja kupitia kichwa na kisha kuingia mwilini. Kwa kuingia mwilini, zinaweza kubadilisha njia zinazotegemea estrogeni, mchakato unaohusika katika kudhibiti kiasi cha estrogeni mwilini ambayo inaweza kusababisha uvimbe wa endometriamu,” ameeleza.

Lakini tunao ushahidi kwamba idadi ya kemikali hizi zinahusishwa na saratani ya matiti na ovari kwa sababu huharibu viwango vya estrojeni mwilini, na hiyo inaweza kuwa njia ambayo inaweza kusababisha viwango vya juu vya saratani ya endometrial (uterine).

Send this to a friend