Utafiti: Watoto wanaotazama televisheni na simu kwa muda mrefu hatarini kupata magonjwa ya moyo

0
140

Watoto wanaotumia muda mwingi wakitazama skrini kama simu au televisheni wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo, matatizo ya metaboli na kisukari kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini Denmark.

Utafiti huo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Copenhagen, ulihusisha watoto zaidi ya 1,000 wenye umri wa miaka 10 hadi vijana wa miaka 18, ambapo watafiti walifuatilia muda wanaotumia kwenye skrini wakichunguza uhusiano kati ya muda wa kutazama skrini na hatari ya matatizo ya afya kama shinikizo la damu, kolesteroli nyingi na kukosa usikivu wa insulini (insulin resistance).

“Mfano, mtoto anayekaa mbele ya skrini kwa saa 3 zaidi kwa siku anaweza kuwa kwenye hatari kubwa ya kupata matatizo ya moyo na kisukari kuliko wenzao,” amesema David Horner, kiongozi wa utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen.

Watafiti wengi bado wanajadili madhara halisi ya skrini kwa watoto na vijana, lakini wengi wao wanakubaliana kuwa watoto wako kwenye hatari zaidi ikilinganishwa na watu wazima.

Send this to a friend