Utafiti: WHO yasema hydroxychloroquine inaongeza vifo kwa wagonjwa vya Covid-19

0
40

Wakati dunia ikiendelea na majaribio ya dawa mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na janga la corona, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesitisha kwa muda majaribio ya dawa ya malaria, hydroxychloroquine, kama moja ya dawa zinazodhaniwa kuweza kutibu Covid-19.

Bodi ya Wakurugenzi ya WHO imechukua uamuzi huo kufuatia utafiti uliochapishwa katika jarida la The Lancet Mei 20 mwaka huu unaoonesha kuwa dawa hiyo inaongeza uwezekano wa vifo kwa wagonjwa wa Covid-19.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema kuwa watafanya mapitio ya dawa hiyo kuweza kujua usalama wake.

Baadhi ya viongozi duniani akiwemo Rais wa Marekani, Donald Trump wamekuwa wakisisitiza kuwa dawa hiyo inawasaida waathirika wa virusi vya corona licha ya kutokuwepo kwa ushahidi wa kisayansi.

Send this to a friend