Uteuzi wa Kijazi: Rais Magufuli asema kuteua ndugu serikalini sio hoja

0
37

Rais Joh Magufuli amesema kuwa kuteua ndugu au watu wanaotoka sehemu moja katika nyadhifa mbalimbali serikalini sio tatizo na kwamba kikubwa ni utendaji kazi wao.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo mapema leo akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu ya Chamwino Dodoma alipokuwa akieleza sababu ya uteuzi wa Kamishna wa Uhifadhi, Dkt. Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na uteuzi wa viongozi wengine wanaotoka eneo moja.

Rais Magufuli amesema kuwa hajamteua Allan Kijazi kwa sababu kaka yake (John Kijazi) ni Katibu Mkuu Kiongozi na kwamba hata wakati wa kumteua hakumwambia kaka yake. Amesema alimteua kwa sababu alikosa mtu wa kushika nafasi hiyo.

“Mtu kuwa ndugu au kutoka sehemu moja is not an issue [sio hoja], issue [hoja] ni perfomance [utendaji kazi] wa mhusika,” amesisitiza Rais Magufuli.

Amesema changamoto kama hiyo amekutana nayo baada ya kuteua watu wawili kutoka Wilaya ya Mbarali, na kwamba jambo hilo limezua maswali kwa sababu nafasi za uteuzi zinapaswa kuangalia uwiano wa nchi.

Send this to a friend