Uteuzi wa viongozi uliofanywa na Rais Samia usiku huu

0
42

Rais wa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo;

  1. Amemteua Prof. Henry Fatael Mahoo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
  2. Amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Dkt. Gerald Ndika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Dkt. Ndika ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
  3. Amemteua Prof. Aurelia K. Kamuzora kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania.
  4. Amemteua Prof. Idris S. Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Tanzania. Prof. Kikula ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Aidha, Rais Samia amewateua Prof. Abdulkarim Mruma na Bi. Janeth Lekashingo kuwa wajumbe wa Tume ya Madini Tanzania.

Uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 20 Aprili, 2021.

Send this to a friend