UTURUKI: Mtoto asimulia alivyoishi siku nne chini ya kifusi akinywa mkojo

0
11

Kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Uturuki na Syria, mvulana mwenye umri wa miaka 17, ambaye alinasa chini ya vifusi siku ya Jumatatu Februari 06, 2023, ameokolewa baada ya takriban siku nne.

Kulingana na ripoti ya ABC News, kijana huyo Adnan Muhammet Korkut amesimulia kuwa alipokuwa amenasa chini ya kifusi alikunywa mkojo wake na kula maua ili aendelee kuishi.

Adnan Muhammet amesema siku ya tukio hilo alikuwa amelala nyumbani na mara tetemeko hilo lilipoanza alitafuta sehemu ya kujibanza ili kujinusuru na maafa hayo.

Amesema aliweka kengele (alarm) kwenye simu yake kwa kila dakika 25 ili asilale lakini baada ya siku mbili, betri ya simu yake iliisha chaji.

Panya road wavamia na kujeruhi wakazi wa Bunju

Ameendelea kusimulia kwamba alikuwa akiwasikia waokoaji lakini sauti yake haikuweza kuwafikia mpaka ilipofika siku ya nne walipoweza kumpata na kumwokoa.

Mpaka sasa takribani watu 22,000 wamefariki dunia kufuatia tetemeko hilo na maelfu ya watu wakikosa makazi huku juhudi za uokozi zikiendelea.

Send this to a friend