Uwanja mpya wa mpira Arusha kupewa jina la Rais Samia

0
92

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema uwanja mpya wa michezo utakaojengwa mkoani Arusha unatarajiwa kupewa jina la Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa mahojiano na kituo cha Wasafi Radio, amesema uamuzi huo ni kuheshimu mchango mkubwa wa Rais Samia katika upande wa michezo, na kwamba pendekezo hilo limebaki kwa Rais Samia kulipitisha.

Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wasimamishwa kutumika Ligi Kuu

Aidha, Msigwa amesema ujenzi huo unaotarajia kuingiza watu 30,000 ni sehemu ya jitihada za Tanzania kuandaa fainali za AFCON 2027 ambazo zitafanyika kwa ushirikiano na nchi za Kenya na Uganda.

Eneo hilo lililopo Kata ya Olmonti mkoani humo lina ukubwa wa ekari 36.1, kwa sasa linamilikiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.