Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wasimamishwa kutumika Ligi Kuu

0
94

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesitisha matumizi ya uwanja wa Jamhuri, Morogoro urushaji wa matangazo mubashara ya runinga.

“Klabu ya Simba ambayo imekuwa ikitumia uwanja huo kwa michezo yake ya nyumbani […] sasa itatumia uwanja wa Azam Complex uliopo Dar es Salaam kwa michezo yake ya nyumbani,” imesema TPLB.

Aidha, TPLB imesema uwanja wa Jamhuri utaendelea kutumika kwa michezo ya mashindano mengine yote yaliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikiwemo Ligi ya Championship ya NBC na First League zinazoendeshwa na kusimamiwa na Bodi ya Ligi Kuu.

Send this to a friend