Uwanja wa Mkapa wafungwa hadi Oktoba 2024, Serikali yaeleza sababu

0
20

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuufunga Uwanja wa Benjamin Mkapa na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mpaka pale ukarabati utakapomalizika Oktoba mwakani.

Wizara imefafanua kwamba viwanja hivyo vilitangazwa kuingizwa katika mpango wa ukarabati mkubwa tangu Julai, 2023 ambapo villipaswa kutotumika kwa michezo ya soka.

“Hata hivyo, kutokana na maombi ya timu zinazocheza ligi kuu na uhitaji mkubwa wa viwanja hivyo kwa ajili ya michuano ya kimataifa, wizara iliridhia ombi la kuendelea kutumika kwa viwanja hivyo wakati ukarabati ukiendelea,” imeeleza taarifa ya wizara.

Serikali imesema kazi ya ukarabati mkubwa inaendelea katika uwanja huo na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Uhuru upo mbioni kuanza baada ya taratibu za kumpata mkandarasi kukamilika.

Aidha, Timu zilizoomba kutumia uwanja huo kama viwanja vyao vya nyumbani zimeelekezwa kutafuta viwanja vingine.