Uwanja wa ndege wa Iringa kukuza utalii na ajira

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi wa Iringa kujiandaa na ajira nyingi zitakazotolewa katika uwanja wa ndege wa Iringa pindi utakapokamilika.

Ameyasema hayo alipokuwa akiweka Jiwe la Msingi  katika mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Iringa na kusalimiana na wakazi wa eneo hilo.

“Nimeambiwa uwanja huu utatoa ajira zaidi ya 150 kwa wana Iringa. Kwa hiyo jipangeni,” amesema.

Rais Samia: Msiwabughudhi wananchi mnapowaomba michango

Aidha, Rais Samia amesema uwanja huo utafungua utalii wa kutosha mkoani humo kutokana na Iringa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo bado havijafunguliwa.

Amebainisha kuwa, baada ya miezi 18 hadi 20 Iringa itaanza kupokea ndege kubwa zinazoweza kubeba abiria kuanzia 70 na kuendelea.

Mbali na hilo, amewaahidi wananchi wa Iringa kuendeleza ujenzi wa kituo cha utalii ambacho kimeachwa kwa muda mrefu kupitia Mradi  wa Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).