UWT yaridhishwa na ujenzi bandari ya Kilwa

0
14

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umesema umeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Kilwa na kuwataka wakandarasi kutekeleza mradi huo kwa wakati kwani wananchi wanategemea kunufaika na mradi huo.

Hayo yamesemwa leo Julai 13, 2023 wakati walipotembelea mradi huo mkoani Lindi wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT, Mary Chatanda na Makamu mwenyekiti UWT, Zainab Shomari pamoja na Kamati ya Utekelezaji.

Aidha, Chatanda ameutaka uongozi wa bandari kuwa na usawa kwenye suala la ajira kwa jinsia zote kwa wanawake na wanaume akibainisha kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na matunda ya nchi yake.

Hata hivyo, amekanusha suala la baadhi ya watu wanaopotosha kwamba bandari ya Dar es Salaam imeuzwa, na kueleza kuwa bandari hiyo haijauzwa kwa mtu yeyote, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini kwakuwa hizo ni harakati za kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 .

“Kuna watu wana nia mbaya na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kupotosha jamii kwamba bandari imeuzwa, niseme ndugu wananchi msiwasikilize hao ni matapeli,” ameeleza.

Ameongeza, “siku zote wakina mama wana nidhamu sana, wana huruma na waangalifu. Wanasema anauza nchi? [Rais] Waogopeni watu wa namna hii wanaokuja kuwadanganya huku, yote haya ni kipindi cha uchaguzi, tunaelekea kwenye uchaguzi.”

Send this to a friend