Valentine’s Day inavyoweza kukusababishia matatizo ya kiakili

0
38

Siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ ambayo huadhimishwa Februari 14 kila mwaka kwa heshima ya Mtakatifu Valentine inakua kila mwaka.

Siku hii huwapa nafasi watu kuoneshana upendo kwa marafiki, familia na wapenzi kwa kupeana maua na zawadi mbalimbali. Hata hivyo, shamrashamra hizi zote za Siku ya Wapendanao pia inaelezwa kuwa zinaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya akili.

Kwa mujibu wa Mwanasaikolojia Mehezabin Dordi, watu walio katika uhusiano wa kimapenzi wanaweza kuhisi kulazimishwa kununua zawadi za bei ghali ili kuwaridhidha wenza wao, huku wale ambao hawajaoa wanaweza kuhisi maisha yao hayajakamilika bila kuwa na wenza, kwa hivyo, katika hali hii mara nyingi siku hii inaweza kuishia kuwa ngumu kiakili.

Anaeleza kuwa baadhi ya watu huathirika kwa kulinganisha uhusiano wao na hadithi za kimapenzi wanazoziona kwenye tamthilia pamoja na jinsi watu wanavyowasilisha mahusiano yao katika mitandao ya kijamii, hivyo kuhisi mahusiano yao hayafai.

“Kihistoria, matangazo mengi yanayohusu Siku ya Wapendanao yamekuwa yakiwalenga hasa wanaume kujitolea kununua zawadi za kifahari na za kupendeza karibu kila wakati kwa wenzi wao. Yote haya huleta msongo wa mawazo usio na usawa kwa wanaume,” anaeleza Mehezabin Dordi.

Anaongeza kuwa Siku ya Wapendanao huathiri kila mtu iwe hajaoa au yuko kwenye uhusiano. Siku hii inaweza kuwakumbusha watu jinsi walivyo wapweke au huzuni na kuwafanya wajisikie vibaya wanapoona wapenzi wengine katika mitandao na jamii kwa ujumla wakifurahia siku hiyo.

Mbinu 5 za kuzungumza kwa kujiamini mbele ya watu wengi

“Moja ya hisia kuu ambazo mtu anaweza kuhangaika nazo ni upweke. Kuhisi upweke si tatizo la afya ya akili peke yake, lakini ni jambo linalohitaji kuangaliwa. Hisia hii inaweza kuwa na sababu nyingi kulingana na hali ya maisha ambayo mtu anakabiliana nayo. Kwa mfano, kuvunjika kwa uhusiano, kufiwa au hata kutoeleweka na mwenza aliyepo,” amefafanua zaidi.

Send this to a friend