Vatican yasema Papa Francis ana dalili za figo kufeli

0
2

Taarifa ya Vatican imesema Papa Francis bado yuko katika hali ya mahututi, huku vipimo vya damu vikionyesha dalili ndogo za kushindwa kwa figo kwa kiwango cha chini ambacho kwa sasa kipo chini ya udhibiti.

Taarifa hiyo imesema madaktari wanatarajia ataendelea kulazwa hospitalini hadi wiki ijayo.

Mapema Jumapili, Vatican ilisema Papa Francis alipatiwa oksijeni kwa kiwango cha juu baada ya kukumbwa na tatizo la kupumua, lakini baadaye alipata nafuu.

Timu ya matibabu ya Papa hapo awali ilisema Ijumaa kwamba hali yake si ya kutishia maisha, lakini bado yuko katika hatari.

Send this to a friend