VETA yabuni miwani ya kumzuia dereva kusinzia

0
35

Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mkoani Dodoma kimebuni mfumo maalum wa kielektroniki wa kudhibiti ajali ikiwemo miwani itakayomdhibiti dereva wa basi asisinzie.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu yanayofanyika jijini hapo, mwalimu wa chuo hicho, Yusuph Haule amesema ubunifu huo utatatua wimbi hilo hasa kwa magari ya mabasi yaendayo mikoani na malori wanaosinzia nyakati za usiku.

“Madereva wengi wanasafiri umbali mrefu, ili kudhibiti ajali zinazotokana na usingizi, tumetengeneza miwani ya kielektroniki ambayo itakuwa inampa taarifa dereva kuwa anasinzia kwa hiyo tumeweka vitu vya kielektroniki kwenye mfumo ambavyo vinahesabu mikonyezo,” amesema.

Mwanadamu ambaye ni mzima anakuwa na mikonyezo ya macho (kufumba na kufumbua) mara 15 hadi 25 kwa dakika moja. Mfumo huu tumetengeneza kwa kuweka controller ambazo zimepewa akili ambayo imepangiliwa na kompyuta kwa ajili ya kudhibiti mikonyezo ya macho.

Kiama kwa Askari wanaoingiza mifugo hifadhini ili wawataifishe 

Amesema dereva akisinzia atapata taarifa mara tano mfululizo na asiposikia mfumo utapunguza spidi hadi kufikia 20 kwa kuwa spidi hiyo si hatarishi na haiwezi kuleta madhara makubwa ikilinganishwa na anapokuwa kwenye mwendokasi.

Sauti hiyo itasikika hadi kwa abiria ikisema kuwa ‘dereva unasinzia kwa usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara simamisha gari lako’ ujumbe huu utarudia mara kadhaa na utaanza kufanya kazi mara moja baada ya dereva kuwasha gari.

Kadhalika amesema kitawekwa kifaa maalum kitakachomzuia dereva kuendesha gari akiwa amelewa na tayari wameshaagiza vifaa hivyo vitakavyowasili hivi karibuni.

Send this to a friend