Vibaka wamkata mapanga na kuiba fedha na simu

0
61

Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni vibaka  wamevamia katika makazi ya Yohana Shija, mkazi wa Mtaa wa 14 Kambalage wilayani Geita mkoani Geita na  kupora kiasi cha laki 3 pamoja na simu tatu za kiganjani, kisha kumjeruhi Shija kwa kumkata mapanga kichwani.

Akizungumza na swahilitimes Shija amesema vibaka hao walivamia nyumbani kwake majira ya  saa 8 usiku baada ya kufanikiwa kubomoa mlango  kwa kutumia jiwe kisha kuingia ndani na kuwalazimisha kutoa pesa.

Mtendaji wa Kata ya Buharahara, Veronica Ntewe amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akisema wameimarisha hali ya ulinzi kwa kufanya ulinzi shirikishi katika maeneo yao kwa lengo la kukabiliana na matukio kama hayo.

Send this to a friend