Vibanda 6,000 vya mashabiki Qatar kupelekwa Kenya

0
41

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Hua Chunying amesema vibanda 6,000 yanayotumiwa na mashabiki nchini Qatar yatatolewa kwa ajili ya matumizi ya watu wasio na makazi nchini Kenya.

Chunying ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba vibanda hivyo vilitengenezwa na kampuni za China ili kutumika kama makao ya muda kwa idadi kubwa ya mashabiki wa soka wanaohudhuria mashindano hayo ya mwezi mmoja.

“Mabanda hayo yalitengenezwa na kkampuni za China, na yatatolewa kwa watu wasio na makazi nchini Kenya baada ya michezo,” ameandika kwenye ukurasa wa Twitter.

Mabanda hayo kwa ajili ya Kombe la Dunia la mwaka huu yako katika mfumo wa vyumba vilivyotengenezwa tayari vyenye ukubwa wa mita 16 za mraba. Vyumba hivi vinaweza kuchukua watu wawili watakaotumika vitanda vya mtu mmoja mmoja, au watu wawili watakaotumia kitanda kimoja cha watu wawili.

Send this to a friend