Video: Mwenye nyumba aezua paa baada ya mpangaji kuchelewesha kodi

0
48

Mama wa watoto nne, raia wa Kenya, amejikuta akiishi katika nyumba isiyo na malango na sehemu ya paa, baada ya mama mwenye nyumba kuvung’oa kufuatia mpangaji huyo kushindwa kulipa kodi ya mwezi Aprili.

Mjane Ruth Shiundu amesema ameshindwa kupata TZS 236,000 ya kodi kufuatia biashara yake ya kuuza mashuka ya mtumba kuathiriwa sana na virusi vya corona.

Mama huyo anayeishi katika chumba kimoja alihamia kwenye nyumba hiyo jijini Nairobi Disemba 2019, na kwa kipindi chote kabla ya Aprili amekuwa akilipa kodi.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Citizen nchini humo amesema kuwa Jumatatu mwenye nyumba alifika na vijana na kung’o mlango, licha ya kuwa tayari alikuwa amemwambia kuwa hana hela, na pindi atakapopata, atamlipa.

Akieleza huku akitokwa na machozi, Shiundu amesema Jumanne mwenye nyumba huyo alifika na kuezua sehemu ya paa la nyumba.

Hapa chini ni taarifa ya tukio hilo;

(Picha: Maktaba)

Send this to a friend