Video: Profesa wa Money Heist akoshwa na waigizaji wa Nigeria walioiga tamthilia hiyo

0
53

Muigizaji nyota wa tamthilia ya Money Heist (Lacasa de Papel) Alvaro Morte maarufu Profesa ameonesha kukoshwa na kikundi cha wavulana kuoka nchini Nigeria kwa namna walivyoigiza upya na kwa ufasaha sehemu ya tamthilia hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Profesa amesema kikundi hicho, Ikorodu Bois, ambacho kimeibua msisimko kwenye mitandao ya kijamii, kimefanya kazi nzuri sana.

“Kazi nzuri sana, pongezi kwenu. Asanteni sana kwa hili. Nyote ninyi mpo vizuri sana,” tafsiri ya alichokiandika Profesa kwa lugha ya Kiingereza.

Kikundi hicho kinachoundwa na ndugu ambao ni Muiz Sanni, 15, Malik Sanni, 10, Babatunde Sanni, 23, na Fawas Aina, 13, kina wafuasi zaidi ya 570,000 katika mtandao wa Instagram na wafuasi takribani 40,000 Twitter.

Wameeleza kikundi chao ni sawa na kikundi cha uchekeshaji, na wamekuwa wakifanya mambo mengi lakini hawakuwa wakiweka mitandaoni.

Send this to a friend