Magombea Urais nchini Kenya, Raila Odinga ametoa video ya wimbo alioshirikishwa, wakati kampeni za uchaguzi nchini humo zikishika kasi.
Odinga ambaye ndiye mpinzani mkuu kwenye uchaguzi huo ametoa video hiyo ya wimbo unaokwenda kwa jina la Leo ni Leo (Remix).
Si jambo la kawaida kuona mgombea urais akitoa wimbo kwa ajili ya kampeni zake, mara nyingi msanii au wasanii anaye/wanaomuunga mkono ndio huimba kwa ajili yake.
Leo Ni Leo the remix. #BabaTheArtist pic.twitter.com/PTcxPFHqWb
— Raila Odinga (@RailaOdinga) February 15, 2022
Remix hiyo imetokana na wimbo wa msanii maarufu kutoka Magharibi mwa Kenya, Emmanuel Musindi, ukanda ambao unaaminika kuwa ni ngome imara ya mgombea huyo.
Hii ni mara yake ya tano akiwani kuingia katika ofisi hiyo ya juu zaidi Kenya, na wengi wakiamini kwamba huenda ikawa mara yake ya mwisho.