Video ya Enjoy ya Jux na Diamond yaondolewa Youtube

0
62

Video ya wimbo ‘Enjoy’ wa mwanamuziki Juma Jux aliyomshirikisha Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnum’ imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kwa sababu ya hakimiliki (Copyright).

Akizungumza na kituo cha Habari cha Mpenja TV, Mwanamuziki kutokea nchini Congo, Sapologuano Odenumz ambaye ndiye aliyeondoa ‘audio’ ya wimbo huo mwezi mmoja uliopita amesema sababu za kuondoa video hiyo ni baada ya msanii Jux kuvunja makubaliano waliyowekeana.

“Tulimalizana kimaongezi na vitu vingine ambavyo tumeongea nao tukamalizana nao siwezi nikaviweka wazi, lakini kuna baadhi ya vitu vingine ambavyo hawakutimiza ndio nimeamua kuishusha tena,” amesema.

Ameongeza, sisi hatuna nao ubaya, mbele ya kufanya kitu chochote huwaga tunawajulisha kwanza, wanapokataa kutujibu tunaona kama hawa watu wanatugeuka na sisi tunafanya ya kwetu.”

Mwezi uliopita msanii huyo alikiri kwamba ni kweli alitoa malalamishi kwa mtandao wa YouTube kufungia audio hiyo kwa sababu melodi za wimbo wake wa ‘I found love’ zilipatikana kwenye wimbo wa Enjoy.