Video ya ngono ya 'Askofu Gwajima' ni feki- Waziri Lugola

0
55

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa video ya ngono iliyosambaa mtandaoni juma lililopita ikidaiwa kuwa ni ya kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, ni ya kutengenezwa.

Kangi Lugola amesema kuwa baada ya wataalamu kutoka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, wamegundua kuwa video hiyo inayodaiwa ni ya Askofu Josephat Gwajima ni ya feki.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na gazeti la The Citizen ambapo amebainisha kuwa hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusu sakata hilo, na uchunguzi bado uanendelea.

Juma lililopita ilisambaa video ya ngono mtandao ikimuonesha sura iliyoaminika kuwa ni ya kiongozi huyo wa kiroho, ambapo taharuki kubwa iliibuka.

Akizungumzia tukio hilo Gwajima alisema kuwa anafahamu video hiyo imetengenezwa kwa makusudi ili kufanya asiongee hasa kutokana na kukaribia kwa uchaguzi mkuu ambao utafanyika nchini mwakani.

Gwajima alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari kanisani kwake, kwamba kwa akili ya kawaida, mtu hawezi kuwa anafanya kitendo kile, ambacho mara nyingi hufanywa kwa siri, yeye ajirekodi halafu asambaze mwenyewe.

Send this to a friend