Vifo vya uzazi nchini vimepungua kwa asilimia 80

0
33

Rais Samia Suluhu Hassan amesema vifo vinavyotokana na uzazi kwa akina mama vimepungua kutoka vifo 530 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2015/2016 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2022.

Ameyasema hayo Oktoba 28, 2028 wakati akizundua Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 pamoja na ugawaji wa magari 216 ya kubebea wagonjwa na magari 153 kwa ajili ya usimamizi na uratibu wa shughuli za afya katika halmashauri nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa JNICC jijini Dar es Salaam.

“Tukilinganisha na shabaha ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) imetuagiza mpaka ikifika mwaka 2030 vifo vitokanavyo na kina mama wakati wa uzazi visizidi 70 kwa vizazi hai laki moja, [..] Safari yetu mpaka 2030 tunaweza tukafikia hili lengo,” amesema.

Mtaalamu: Hakuna Majibu ya Malaria 1, 2 au 3, wataalamu wanakiuka 

Aidha, amesema serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kununua vifaa vya kisasa na kusomesha madaktari ili kutoa huduma bora na kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi ya vifo vya watoto imepungua kwa asilimia 1 pekee.

Ripoti hiyo inaonesha pia idadi ya mimba za utotoni imepungua kutoka asilimia 27 mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 22 mwaka 2022 huku kiwango cha udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 kikipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2015/2016 hadi asilimia 30.

Send this to a friend